Mustafa, kiungo mahiri wa Buffalo FC, amefunguka baada ya mechi dhidi ya Alliance FC, akieleza kuwa ilikuwa changamoto kubwa kwao kutokana na maandalizi na nidhamu ya wapinzani wao. Alieleza kuwa Alliance walicheza kwa umakini mkubwa, wakizuia mashambulizi na kulazimisha Buffalo kufanya kazi ya ziada kutafuta nafasi ya ushindi. Hata hivyo, anasema timu yao ilipambana hadi dakika ya mwisho na kujifunza mambo mengi kutoka katika mechi hiyo. Mustafa alimalizia kwa kuahidi mashabiki wao kuwa Buffalo FC itaendelea kujipanga ili kufanya vizuri zaidi katika mechi zijazo.
MUSTAFA MCHEZAJI WA BUFFALO FC ASEMA: METCH DHIDI YA ALLIANCE ILIKUA NGUMU – WALIJIPANGA VIZURI
