Ethiopia yasema imewakamata wanachama wa ISIS waliopata mafunzo nchini Somalia

Mamlaka nchini Ethiopia imetangaza kuwakamata washukiwa 82 wa kundi la Islamic State, ambao waliripotiwa kuwa wamepewa mafunzo ya kutekeleza mashambulizi ya kigaidi nchini humo.

Taarifa iliyotolewa na Shirika la Kitaifa la Ujasusi na Usalama la Ethiopia (NISS) Jumatatu ilisema watu waliokamatwa wanahusishwa na mrengo wa ISIS unaoendesha shughuli zake nchini Somalia.

Inasemekana walipata mafunzo huko Puntland, eneo linalojitawala kaskazini mashariki mwa Somalia, kabla ya kutawanywa katika mikoa mbalimbali ya Ethiopia – ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa Addis Ababa, eneo la Amhara, na eneo la Oromia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *