Lamine Yamal mashakani kuhusiana na mzozo wa walemavu .

izara ya Haki za Kijamii ya Uhispania imeitaka ofisi ya mwendesha mashtaka wa nchi hiyo kumchunguza winga wa Barcelona Lamine Yamal baada ya kuripotiwa kuwaajiri watu wenye ulemavu kutumbuiza kwenye sherehe yake ya kutimiza miaka 18.

Lamine Yamal aliandaa karamu siku ya Jumapili katika nyumba iliyokodishwa huko Olivella, mji mdogo ulio kilomita 50 kaskazini magharibi mwa Barcelona, na wageni wakiwemo WanaYouTube, washawishi, na wachezaji wenzake kadhaa wa Barcelona.

Inadaiwa Lamine Yamal alikodisha kikundi cha watumbuizaji walio na ulemavu, jambo ambalo Chama cha Watu wenye Achondroplasia na Dysplasias nyingine za Mifupa nchini Uhispania (ADEE) kilieleza kuwa “halikubaliki katika karne ya 21”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *