Sakata la Rasilimali za CHADEMA: Mawakili Wadai Msajili Amepotosha Hukumu

Mawakili wa Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA na Katibu Mkuu wa chama hicho wamepinga vikali ‘uhalali’ wa barua iliyoandikwa na Msajili wa Mahakama ya Tanzania kwenda kwa Mawakili wa Saidi Issa Mohamedi, na wenzake wawili inayolenga kufafanua kuhusiana na uamuzi uliotolewa na Mahakama hiyo juu kuhusiana na marufuku ya matumizi ya rasilimali za chama.

Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es Salaam leo, Jumamosi Julai 19.2025 Wakili Hekima Mwasipu amesema Mawakili watatu wanaoiwakilisha CHADEMA katika kesi hiyo ambao ni Hekima Mwasipu, Dkt. Rugemeleza Nshala na Mpale Mpoki walipigiwa simu na Naibu Msajili wa Mahakama wakielezwa kuwa wanapaswa kutuma anuani zao ili watumiwe barua kutoka kwa Msajili wa Mahakama, na walipofanya hivyo walipokea nakala ya barua (kupitia email) inayoeleza ufafanuzi wa uamuzi huo, ambapo barua hiyo ilionesha orodha ya watu 10 waliopigwa marufuku kujishughulisha na shughuli zozote za chama kwa namna moja au nyingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *