Donald Trump anaugua ugonjwa sugu wa mshipa, Ikulu ya Marekani ilitangaza siku ya Alhamisi, baada ya siku kadhaa za uvumi kuhusu picha zinazoonyesha michubuko kwenye mkono wa rais huyo wa Marekani.
Baada ya hivi karibuni kupata uvimbe kwenye miguu yake, Trump alifanyiwa “uchunguzi wa kina” ikiwa ni pamoja na upimaji wa mishipa ya damu, kulingana Msemaji wa Ikulu Ikulu ya Marekani Karoline Leavitt.
Leavitt alisema hali ya mkono wa Trump ulioonekana kuvimba ilitokana na “uharibifu wa tishu kutokana na kusalimiana kwa mara kwa mara” wakati akitumia dawa ya aspirini, ambayo alisema ni “sehemu ya utaratibu wa kawaida wa kudhibiti moyo na mishipa”.