“Watangazaji hao hawajasajiliwa na kupewa Ithibati na Bodi, hivyo wanafanya kazi za kihabari kinyume na Kifungu cha 19 cha Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229
(Toleo la 2023);Watangazaji hao walikiuka haki ya faragha na kutweza utu wa mhojiwa kwa kumlazimisha kutoa tarifa binafsi bila ridhaa yake kinyume na Kanuni ya 11(1)(e) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Utangazaji ya Redio na Televisheni), 2018 (kama zilivyofanyiwa marekebisho); na
Watangazaji hao walitumia lugha ya kumshushia hadhi mhojiwa kinyume na Kanuni ya 11(1)(f) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Utangazaji ya
Redio na Televisheni), 2018 (kama zilivyofanyiwa marekebisho) na Kanuni ya 16(1), ikisomwa pamoja na Jedwali la Tatu aya ya 2(b) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Mtandaoni), 2020.Kutokana na ukiukwaji huo mkubwa wa Sheria na maadili ya taaluma ya habari, Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, imewapiga marufuku watangazaji tajwa hapo juu kujihusisha na masuala ya kihabari kuanzia tarehe 18 Julai, 2025 mpaka hapo watakapotimiza matakwa ya Sheria ikiwa ni pamoja na kuwa na sifa za kielimu na kuzingatia maadili ya taaluma ya habari.Bodi inatoa ony kali kwa watu wote wanaofanya kazi za kihabari kuhakikisha kuwa wanazingatia matakwa ya Sheria kwa sababu taluma ya habari ni mhimili muhimu wa utawala bora unaotegemea ukweli, uadilifu na heshima kwa utu a binadamu.”
Watangazaji wa Mjini Fm Kufungiwa na Bodi ya Ithibati
